Jan 13, 2015

Hongereni kwa kuwadhibiti Mapandikiz;Maalim Seif

Wanachama wa

chama cha wananchi CUF Wa kata ya Tandale kwa mkunduge manispaa ya Kinondoni jijini Dar es alaam,wamepongezwa kwa kuweza kuwadhihiti mapandikizi ya CCM Na kuwezesha kushinda mitaa mitatu kati ya mitaa sita iliyopo ndani ya kata hiyo.po

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa chama cha wananchi maalim self sharif hamad,alipokua ana wahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho kwa kukipa ushindi.

Amesema juhudi zenu za kuwadhihiti mapandikizi wakati wa kuandikisha, na wakati wa kupiga kura, ndiyo zilizoipatia ushindi chama chetu.

Ndugu wananchi napenda mufahamu kwamba CCM haiwezi kushinda bila ya kutumia mapandikizi,wakati wa kujiandikisha na wakati wa kupiga kura.

Aliendelea kusema kwamba ninazo taarifa,muliwadhibiti vilivyo hawa mapandikizi na mumekua ni mfano mkubwa katika Mkoa wa Dar es salaam,kwa kweli nawapongeza kwa hili.mwisho wa kumnukuu.

Aidha aliwaasa wananchi na wanachama wa CUF kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili wawe na haki ya kuchagua viongozi wao katika uchaguzi utakaofanyika Mwishoni mwa mwaka huu.


Mkutano huo ulifanyika jioni hii na kuhudhuria na mamia ya wapenzi wa chama hicho

0 comments:

Post a Comment