Nov 23, 2014

Wanamgambo 60 wa Kijerumani wauawa Iraq na Syria

Mkuu wa Ofisi ya Kulinda Katiba ya Ujerumani amesema kuwa, raia wa nchi hiyo wasiopungua 60 ambao walijiunga na kundi la kigaidi la Daesh wameuawa nchini Syria na Iraq.
Hans-Georg Maassen amesema kwamba, inakadiriwa kuwa Wajerumani 60 wameuawa au kujilipua katika mashambulizi ya kundi la Daesh huko Iraq na Syria na kutahadharisha kwamba, Ujerumani inapaswa kujitayarisha iwapo wanamgambo kama hao waterejea nyumbani.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Thomas de Mairiziere alisema Novemba 20 kwamba, Wajerumani wasiopungua 550 wameondoka nchini humo kwenda kujiunga na kundi la kitakfiri la Daesh linalozusha machafuko katika nchi za Mashariki ya Kati.

 Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwezi Oktoba na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, raia wa kigeni 15,000 wameelekea nchini Syria na Iraq kushiriki katika mapigano ya kundi la kitakfiri la Daesh au makundi mengineyo ya kigaidi.

0 comments:

Post a Comment