Nov 23, 2014

Jeshi la Kenya kuwasaka wauaji Mandera mpakani mwa Somalia

Bus lililotekwa na wapiganaji wa Al shabab kabla ya kuwaua abiria 28 wasiokuwa waislamu,Mandera mpakani mwa Somalia
Bus lililotekwa na wapiganaji wa Al shabab kabla ya kuwaua abiria 28 wasiokuwa waislamu,Mandera

Mshauri wa juu wa raisi Uhuru Kenyata Abdikadir Mohammed ametoa wito kwa wakenya wote wa imani zote kuungana pamoja dhidi ya wahalifu.

Hatua hiyo inakuja kufuatia mauaji ya alfajiri ya jana kutekelezwa na wapiganaji wa kiislamu kutoka somalia ambao waliteka basi moja na kuwaua abiria ambao hawakuwa waislamu.

Tayari maafisa wa jeshi la Kenya KDF wamewasili Mandera eneo la mpakani mwa somalia kuwasaka waliotekeleza mauaji hayo na kuhakikisha ulinzi baada ya abiria 28 kuuawa mapema jana.

Kundi la Al-Shabab limesema shambulizi hilo lililenga kulipa kisasi kufuatia mauaji ya waislamu ambayo kundi hilo limedai kutekelezwa na majeshi ya kenya katika mji wa pwani wa Mombasa.

Serikali ya kenya imesema imeanza kuwatambua wahalifu hao na itahakikisha inafikisha mbele ya sheria.

Waziri wa mambo ya ndani Joseph Olellenku amesema kuwa kambi iliyokuwa inamilikiwa na wapiganaji hao huko mandera imeshambuliwa na jeshi la kenya.

0 comments:

Post a Comment