Wafanya magendo ya binadamu
wanawatumia vibaya wakimbizi Waislamu wanaokimbia mauaji na unyanyasaji
wa kuchupa mipaka nchini Myanmar.
Televisheni ya Press TV imeripoti leo kuwa, Waislamu wa kabila la Rohingya wa Myanmar ni moja ya jamii za watu wachache ambao wanadhulumiwa na kunyanyaswa vibaya mno na ndio maana wamelazimika kukimbilia nchi nyingine.
Suala hilo limewatia tamaa wafanya magendo ya wanadamu na wanawatumia vibaya Waislamu hao walioporwa utaifa na uraia wao.
Waislamu wengi wa Myanmar wanapoteza
maisha yao njiani wakati wanapokimbia mauaji na mateso ya kupindukia
nchini mwao.
Zaidi ya Waislamu 19 elfu wameshakimbia nchi yao ya Myanmar tangu mwezi Oktoba mwaka huu.
Waislamu hao wananyimwa hata haki
za kimsingi kabisa kama vile uraia, kuoa na fursa ya kiuchumi za
kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya lazima maishani.
Ripoti za Umoja wa
Mataifa na za mashirika ya haki za binadamu zinaonesha kuwa, tangu mwaka
2012 hadi hivi sasa, idadi kubwa ya Waislamu wa Myanmar wameuawa na
kuteswa vibaya na mabudha wenye misimamo mikali.
0 comments:
Post a Comment