Nov 30, 2014

Mahakama moja ya Alexandria nchini Misri yachomwa


Baadhi ya waandamanaji wakipambana na polisi nchini Misri Baadhi ya waandamanaji wakipambana na polisi nchini Misri
Watu wasiofahamika leo wameichoma moto mahakama moja katika mji wa Alexandria nchini Misri. 

Watu hao wasiofahamika wamelichoma moto jengo la mahakama moja katika mji wa Alexandria ikiwa ni kuendelea ghasia za wananchi baada ya kutolewa uamuzi wa kumtoa hatiani dikteta Hosni Mubarak, dikteta wa zamani wa Misri, wanawe wawili, Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati wa utawala wake na manaibu wake kwa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili za kuwaua wafanya maandamano katika Mapinduzi ya wananchi ya mwezi Januari mwaka 2011.
Wakati huo huo mji wa Alexandria umeshuhudia milipuko miwili katika mahakama ya al Munshiya na katika klabu ya majaji katika mji huo na hivyo kusababisha kufungwa baadhi ya barabara. 

Vikosi vya usalama vya Misri jana iliwatia nguvuni baadhi ya watu waliokuwa na lengo la kuandamana katika meidani ya at Tahrir ili kulalamikia uamuzi huo wa mahakama.

0 comments:

Post a Comment