Sixtus Kimaro enzi za uhai wake
MTUHUMIWA
wa kesi ya kulawiti mtoto wa kiume, aliyekuwa akitafutwa na Mahakama ya
Rufaa, Sixtus Kimaro, ambaye alikutwa na tuhuma hizo wakati akiwa Padri
katika Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, amefia nchini
Msumbiji na mwili wake umesafirishwa kuja Dar es Salaam.
Taarifa za kifo
cha Kimaro zilifikia gazeti hili jana kuwa mwili wa Kimaro, ulikuwa
umeshafikishwa katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Lugalo.
Baadaye taarifa hizo zilithibitishwa na Katibu wa Askofu
Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Padri Denis Wigila. Akizungumza na
gazeti hili, Padri Wigila alisema Kanisa limepata taarifa za kifo hicho
kilichotokea nchini Msumbiji.
“Kimaro siyo Padri, kwani aliishaacha
kuwa Mlei, hivyo Kanisa halishiriki katika utaratibu wa mazishi
kikanisa,” alisema Padri Wigila.
Padri Wigila alisema taratibu
za mazishi, zinafanywa na familia ya marehemu kama ilivyo kwa muumini
mwingine, na familia hiyo inatarajia kusafirisha mwili wake leo kwenda
mkoani Kilimanjaro kwa maziko.
Kwa upande wake, Msemaji wa
Baraza Kuu la Maaskofu (TEC), Padri Anatoly Salawa, alipohojiwa kuhusu
tukio hilo, alisema walipata taarifa ya kifo hicho na kuelezwa kuwa
mwili wa marehemu ulikuwa ukitokea nchini Msumbiji na kupelekwa katika
Hospitali ya JWTZ Lugalo.
Kutoroka
Julai mwaka huu,
Mahakama ya Rufaa ilishindwa kusikiliza rufaa ya Jamhuri dhidi ya
Kimaro, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na baadaye kuachiwa na
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Kushindwa
kusikilizwa rufaa hiyo, kulitokana na Kimaro kutokujulikana alipo, kwa
vile alishaacha kutoa huduma katika kanisa hilo.
Kabla ya hatua
hiyo, Wakili wa Serikali, Salum Malick alieleza kuwa wamepata taarifa
kwa Msajili wa Mahakama hiyo, kwamba mhusika alipelekewa hati ya wito
kwa mwajiri wake, Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, lakini
waliambiwa kuwa kwa sasa Kimaro siyo mwajiriwa wao tena na hawajui
mahali alipo.
Jela
Kimaro alihukumiwa kwenda jela
miaka 35 katika kesi ya msingi namba 786 ya mwaka 2005, iliyokuwa
ikimkabili, ambapo alikuwa na mashitaka matatu, yakiwamo ya kumlawiti
mtoto wa kiume wa miaka 17, shambulio la aibu na kumdhalilisha mtoto
huyo.
Padri huyo alikamatwa na askari Polisi wa doria Mei 18,
2005 usiku katika eneo la Changanyikeni jijini Dar es Salaam, ambapo
katika kesi yake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Pelagia
Khaday, Agosti 9, 2006, alimtia hatiani kwa mashitaka yaliyokuwa
yakimkabili.
Kimaro baada ya kupatikana na hatia katika makosa
yote, alihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 35 jela. Katika kosa la
kwanza alihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, na katika kosa
la pili alihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela na
akaamuriwa kumlipa mtoto huyo fidia ya Sh milioni mbili.
Kuachiwa
Hata
hivyo, Kimaro alikata rufaa Mahakama Kuu ambayo ilisikilizwa na Jaji
Robert Makaramba, akipinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu. Katika hoja
zake alidai kuwa Jamhuri haikutoa ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani
kwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.
Jaji Makaramba
alikubaliana na rufaa hiyo na Machi 14, 2008, alimwachia huru akisema
kuwa ameridhika kwamba hapatakuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia
hatiani.
Jaji Makaramba alisema kuwa hitimisho lake katika
hukumu yake kulingana na muda na mahali mjibu rufani na mtoto huyo
walikokutwa, ni ushahidi wa kimazingira.
Alisisitiza kuwa
shahidi wa pili na wa tatu wa mashitaka, ambao ni askari waliodaiwa
kumkuta Kimaro akitenda kosa hilo na mtoto huyo, hawakueleza kwa uhakika
kile ambacho mjibu rufani alikuwa akikifanya.
Jamhuri katika rufaa yake, iliwasilisha jumla ya hoja saba kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya kumwachia huru Kimaro.
Serikali
katika hoja zake, ilidai Jaji aliyesikiliza rufaa hiyo, pia alikosea
kisheria na kiukweli kueleza kuwa hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja
wa nini mjibu rufani alikuwa akifanya eneo la Changanyikeni Dampo.
Jaji
huyo aliyesikiliza rufaa, alidaiwa kuwa alikosea kisheria na kiukweli
kwa kutotambua ushahidi wa shahidi wa nne katika mashitaka hayo, bila
kutoa sababu zenye nguvu na kwamba alikosea kisheria kwa uamuzi wake
kuegemea kwenye ushahidi wa mazingira.
Aidha, upande wa Serikali
ulieleza kuwa Jaji huyo alikosea kisheria kueleza kuwa shahidi wa nne
wa mashitaka na mjibu rufani, walilazimishwa na uchunguzi wa kitabibu na
kwamba Fomu ya Polisi Namba 3 (PF3) iliyowasilishwa mahakamani, ilikuwa
ni kusudi la utambuzi tu.
Katika hoja hizo za Serikali, Jaji
huyo alidaiwa kupotosha kwa kuhusisha sheria inayohusu ushahidi wa
kimazingira na kwamba alikosea kisheria na kiukweli kusema kuwa hapakuwa
na ushahidi wa kuunga mkono ushahidi wa shahidi wa nne.
Pia,
Serikali ilidai kuwa Jaji aliyesikiliza rufaa, alikosea kisheria na
kiukweli kueleza kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha
Nov 18, 2014
PADRI AKIYETAFUTWA KWA KOSA LA KULAWITI AFARIKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment