Nov 18, 2014

Mtu mmoja asababisha maafa Nigeria

nigeria
Zaidi ya watu 13 wamefariki na 65 wamejeruhiwa vibaya  baada ya mtu wa kujitolea mhanga kujilipua katika soko la simu katika mji wa Azare kaskazini mwa nchi ya  Nigeria.

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo ni kuwa mshambulizi huyo alionekana akiingia sokoni  huku akifuatiwa na manaume wawili ambao mmoja wao aliuawa na wananchi waliokuwa na ghadhabu  baada ya tukio hilo na mwengine akiwa mikononi mwa polisi.

Ikikumbukwa kuwa kisa  hicho ni cha tatu kushuhudiwa nchini humo baada ya mashambulizi mengine ya  kujilipuwa kutokea  katika maeneo tofauti  katika wiki tatu zilizopitata

Uchungunguzi  wa tukio hilo umeshaanzishwa na maafisa wa kitengo cha ujasusi huku yale matukio mengine yakiendelea na uchunguzi.

0 comments:

Post a Comment