Nov 18, 2014

IS yakiri kumkata kichwa Peter Kassig

Peter Kassig, mgambo wa zamani wa jeshi la Marekani, na mateka wa Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Peter Kassig, mgambo wa zamani wa jeshi la Marekani, na mateka wa Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam limetangaza jumapili Novemba 16 kuwa limemkata kichwa mateka wa Marekani Peter Kassig, aliyetekwa nyara mwaka 2013 nchini Syria.

Kundi hilo limerusha hewani video ya dakika zaidi ya kumi na tano ikionesha mtu aliye funikwa uso akisimama karibu na kichwa kiliyokatwa, akisema kuwa amemkata kichwa mateka wa Marekani, Peter Kassig.

Uso wa mateka huyo wa Marekani ulionekana mwisho wa video ya mateka wa Uingereza Alan Henning aliye katwa miezi ya hivi karibuni. 

Wakati huo wapiganaji wa Dola la Kiislam waliahidi kumkata kichwa, Peter Kassig, iwapo Marekani haitositisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya ngome zao. 

Peter Kassig, mwenye umri ya miaka 26, akiwa pia mfanyakazi kwenye shirika moja la kihisani, alikuwa kizuizini kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mwenye asili ya Indiana, mgambo wa zamani wa jeshi la Marekani, Peter Kassig alishiriki upande wa jeshi la Marekani katika vita nchini Iraq mwaka 2007, kabla ya kuanzisha shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wa Syria.

Peter Kassig aliamua kuishi Libanon na Uturuki, ili aweze kuwasaidia wakimbizi wa ndani wa Syria, kwa kuwapatishia chakula na dawa. 

Peter Kassig alitekwa nyara kwenye barabara ya mashariki mwa Syria Oktoba 1 mwaka 2013. 

Tangu wakati huo Peter Kassig alibadili dini na kuwa Muislam, na alikua akiitwa Abdul Rahman.

Mapema mwezi Oktoba, baada ya mauaji ya Alan Henning, wazazi wa Peter Kassig waliwaomba watekaji nyara kumuachia huru mtoto wao.


Peter Kassig ni mateka wa tano kutoka mataifa ya magharibi kuuawa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Wakati huohuo Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam wamekiri kuwaua wanajeshi 15 wa Syria.

Waziri mkuu wa Uingereza ameelezea masikitiko yake juu ya mauaji ya kijana huyo, huku Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls akielezea kutiwa wasiwasi na mauaji hayo ya kinyama. 

Kwa upande wake rais wa Ufaransa François Hollande amesema kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam wamekua wakitekeleza “uhalifu dhidi ya ubinadamu".

0 comments:

Post a Comment