Nov 7, 2014

Mahakama ya kilele yavunja bunge 'halali' la Libya

Mahakama ya kilele nchini Libya leo Alhamisi imetangaza kulivunja bunge linalotambuliwa kimataifa na hivyo kubatilisha uhalali wa serikali ya Waziri Mkuu, Abdullah al-Thani.
Uamuzi wa mahakama hiyo umetolewa baada ya mbunge mmoja kuomba mchakato wa uchaguzi wa Juni 25 uliopelekea kuchaguliwa wabunge wapya uchunguzwe. 

Mahakama ya kilele ya Libya imebaini kwamba uchaguzi wa bunge wa Juni 25 ulikiuka sheria na kwamba haukufanyika inavyotakiwa kikatiba. 

Bunge jipya la Libya limekuwa likifanya vikao vyake katika mji wa mashariki wa Tobruk kutokana na kuendelea ghasia na rangaito katika mji mkuu, Tripoli. Huku hayo yakijiri, bunge lililomaliza muda na ambalo linaendelea kudai kuwa ndilo lenye mamlaka ya kikatiba limesema litatangaza mwelekeo wa kisiasa wa Libya baada ya kuvunjwa bunge hasimu.
 
Libya imekuwa na mabunge mawili tangu mwezi Juni mwaka huu huku machafuko yakiendelea kuigubika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kwa mwaka wa tatu mtawalia tangu kuondolewa madarakani na kisha kuuawa kanali Muamar Gadafi mwaka 2011.
MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014 Written By kunta kinte on Wednesday, November 5, 2014 | 10:52 AM ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU

Make money by copying the best: http://bit.ly/best_tips

0 comments:

Post a Comment