Mahakama ya jimbo la St. Gallen
nchini Uswisi imefuta hukumu ya kupiga marufuku kuvaa Hijabu msichana
mmoja wa shule mwenye umri wa miaka 13 katika skuli moja iliyoko
kaskazini mwa jimbo hilo.
Hakimu wa mahakama hiyo sambamba na kukubali
mashtaka ya wakili wa mwanafunzi huyo Muislamu kwamba uamuzi wa shule
hiyo umekinzana na haki ya kuabudu kwa mujibu wa sheria ya kifederali ya
Uswisi na pia Mkataba wa Haki za Binadamu, ameondoa marufuku ya Hijabu
aliyokuwa amewekewa msichana huyo.
Hakimu wa kesi hiyo pia amesema,
hakujathibitishwa ukiukwaji wowote wa sheria za shule uliosababishwa na
kuvaa Hijabu msichana huyo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, nchini
Uswisi kuna Waislamu laki 4 ambao ni sawa na asilimia 5 ya wananchi
milioni 8 wa nchi hiyo ya bara la Ulaya.
0 comments:
Post a Comment