Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo
mjini Tehran amesema kuwa, kufanyika kura ya maoni kwa ajili ya
kuainisha mustakbali wa Bahrain ndiko kutakodhamini haki muhimu za
wananchi wa nchi hiyo.
Ayatullah Muvahedi Kermani pia amelaani
mashambulio ya askari wa Israel katika msikiti wa al Aqswa na kusema
kuwa, kuendelea jinai za Wazayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu
za Palestina kutapalekea kuanza Intifadha nyingine.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini
Tehran vilevile amegusia ripoti za Ahmad Shahid, Ripota Maalumu wa
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusiana na Iran, na
kusema kwamba kama Ahmad Shahid angekuwa anafuatilia kweli haki za
binadamu, alipaswa kwenda Ukanda wa Gaza au Syria na kusikiliza wanawake
na watoto wasio na hatia wa maeneo hayo wanaoishi katika hali ngumu
kutokana na vitisho vya askari wa utawala ghasibu wa Israel na magaidi.
0 comments:
Post a Comment