Utawala wa Kizayuni wa Israel
umesema kuwa utaruhusu Wapalestina wa marika yote kusali katika msikiti
mtukufu wa al Aqswa, baada ya kupata mashinikizo kwa kuzuia Wapalestina
wasiingie kwenye msikiti huo.
Msemaji wa Polisi ya Israel Mickey
Rosenfeld amesema leo kuwa, hakutakuwa tena na kizuizi cha umri katika
kuingia wafanyaibada wa Palestina katika msikiti wa al Aqswa, kwa mara
ya kwanza baada ya miezi kadhaa.
Hata hivyo ameongeza kwamba vikosi
zaidi vya polisi vimepelekwa huko Mashariki mwa Quds mapema leo.
Maafisa wa Israel wameeleza kwamba,
marufuku hiyo imeondolewa kufuatia mazungumzo ya hivi karibuni kati ya
Mfalme Abdullah II wa Jordan na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa
Israel Benjamin Netanyahu.
Kwa wiki kadhaa msikiti huo mtukufu kwa
Waislamu duniani umegeuka kuwa sehemu ya makabiliano kati ya waumini wa
Kipalestina, walowezi wa Kizayuni na askari wa utawala haramu wa Israel.
Machafuko yalianza mwezi uliopita baada ya Israel kuwazuia wanaume
wenye umri wa chini ya miaka 50 kuingia kwenye msikiti huo, baada ya
Mzayuni mwenye siasa kali Yehuda Glick kuuliwa na watu wasiojulikana.
0 comments:
Post a Comment