Dec 1, 2014

WAZAZI WATAKIWA KUTOOGOPA GHARAMA ZA ELIMU

Watoto wakiswali swala ya jamaa ikiwa ni sehemu ya mafunzo wanayopata kituoni hapo.

swala hiyo iliongozwa na mtoto Mukhtaar Juma.

Wazazi nchini wametakiwa kutoogopa gharama za elimu kwani matunda ya elimu kamwe hayalingani na gharama za elimu.


Wito huo umetolewa jana na Mgeni Rasmi Ndugu Mustwafa Muro ambaye alikua anazungumza na wazazi  katika mahafali ya wakhitimu wa elimu ya awali ya kituo cha Munira kilichopo Magomeni Makuti Jijini Dar es salaam.

Amesema kumekua na kasumba kwa baadhi ya wazazi kuogopa au kukwepa kugharamia elimu ya watoto,kitu ambacho si sahihi.

Akifafanua zaidi alisema kwamba gharama za kuwasomesha watoto licha ya kua ni kubwa lakini hazifanani kabisa na thamani ya elimu.

Kwa upande mwengine aliwataka wazazi kuwaunga mkono walimu na viongozi wa munira nursery kwani watoto wameonyesha ya kuwa wamefundishwa vyema kitaaluma na kimaadili.

"Kwa kweli nimefurahi sana,watoto wadogo sana wameswali vizuri,wamesoma Qur aan tena sura kubwa kubwa,wamesoma risala bila kigugumizi,hii ni dhahiri kwamba kituo hiki kinafundisha vizuri sana,sasa ni jukumu lenu wazazi kuthamini juhudi za walimu hawa"mwisho wa kumnukuu.

awali akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake,mtoto Mukhtaar Juma mbali ya mambo mengine alizitaja changamoto zinazo kikabili kituo kua ni pamoja na uhaba wa magodoro,viti na meza.

Jumla ya wanafunzi saba kati ya wanafunzi 33 wa kituo hicho wamekhitimu na kutoa fursa ya kuanza elimu ya msingi hapo mwakani.

munira day care and english medium ni kituo kinachotoa elimu ya awali kwa watoto kuanzia miaka mitatu hadi sita.

aidha kituo hiki ambacho kinatumia mchepua wa kiingreza kipo magomeni makuti mtaa wa kidugalo.


Kutoka kushoto ni Sheikh Mazoea ambaye ni mwenyekiti serikali ya mtaa makuti A,katikatiMustwafa muro ambaye alikua mgeni Rasmi, na kulia ni Ustaadh Juma Rashid ambaye ni Mkurugeni wa Kituo hicho wakifuatilia kwa makini matukio yakiyofanywa na wanafunzi hao



watoto wakisujudi





0 comments:

Post a Comment