Nov 23, 2014

Kenya: wasafiri 28 wauawa kwenye mpaka wa Somalia

Wapiganaji wa Al Shabab wamekiri kutekeleza shambulio mapema Jumamosi Novemba 22 asubuhi lililogharimu maisha ya wasafiri 28.
Wapiganaji wa Al Shabab wamekiri kutekeleza shambulio mapema Jumamosi Novemba 22 asubuhi lililogharimu maisha ya wasafiri 28.

Abiria 28 wameuawa mapema Jumamosi Novemba 22 asubuhi katika shambulio lililotokea nchini Kenya karibu na mpaka wa Somalia. 

Abiria hao waliyo kuwa ndani ya basi wameshambuliwa na wanamgambo wa Al shabab kutoka Somalia, ambao wamekiri kutekeleza shambulio hilo.

Wanamgambo hao waliwakata vichwa abiria ambao hawakua “waislam”.

Shambulio hilo lilitokea saa 11 na dakika 45 asubuhi, wakati basi hilo likitokea Mandera, mji ambao unapatikana kati ya Kenya, Somalia na Ethiopia, katika eneo la Arabia.

Inasadikiwa kuwa basi lililazimika kusimama, kwani lilikua likilengwa kwa risasi na kusababisha watu wengi waliokua ndani ya basi hilo kujeruhiwa. 

Wauaji hao waliwatenganisha abiria Waislam na wasio Waislam, na baadae kuanza kushambulia abiria wasio Waislam, ambao wengi wao walikua walimu wakirudi makwao kuheherekea sikukuu ya Krismasi,wafanyakazi wa sekta ya afya, watumishi wa umma. 

Jumla ya abiria 28 wakiwemo wanawake 9, kwa mujibu wa mkuu wa Polisi ya Kenya, David Kimaiyo, wameuawa.
 
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limethibitisha idadi hiyo. 

Timu za wafanyakazi wa Idara za dharura wametumwa katika eneo hilo ili kuchukua miili ya abiria waliouawa. 

Viongozi kwa upande wake, wamehakikisha kwamba jeshi limetumwa katika eneo la tukio ili kuwasaka wahalifu.

Utaratibu uliyotumiwa ni sawa na ule uliyotumiwa Mpeketoni katika eneo la Lamu mwezi Juni na Julai ambapo washambuliaji waliwataka watu kutamka nguzo ya kwanza ya uislam "Shahada". Lakini wakati huo, wanaume ndio waliolengwa, wanawake hawakulengwa.

Kundi la Al Shabab limekiri kutekeleza shambulio hilo, likibaini kwamba operesheni hiyio ni ulipizaji kisasi dhidi ya opereshi ya polisi iliyoendeshwa hivi karibuni katika mji wa Bandari ya Mombasa, operesheni ambayo ililenga Misikiti kadhaa iliyochukuliwa kama inafunza imani kali za kidini. 

Wakati huo mamia ya waislam walikamatwa katika operesheni hiyo ya polisi.

0 comments:

Post a Comment