Mapigano ya kuania mji wa Kobane nchini Syria
Nchi za ushirika unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu, IS, zimefanya mashambulizi kaskazini ya Syria zikisaidiwa na vikosi vya Wakurdi katika mji wa Ain al-Arab
Wanamgambo wa itikadi kali wa IS walikuwa umbali wa kilomita tatu tu
mashariki ya mji huo ambao kwa kikurd unajulikana kama Kobané,karibu na
mpaka na Uturuki-kwa mujibu wa shirika la Syria linalochunguza masuala
ya haki za binaadam ,lenye mkao yake nchini Uingereza-shirika
linalokusanya maelezo kutoka duru za kijamii,hospitali na pia kijeshi
nchini Syria.Nchi za ushirika unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu, IS, zimefanya mashambulizi kaskazini ya Syria zikisaidiwa na vikosi vya Wakurdi katika mji wa Ain al-Arab
Ushirika wa Marekani na nchi za kiarabu" wamefanya hujuma zaidi ya mara tano dhidi ya vituo vya wanamgambo wa itikadi kali katika uwanja wa mapambano,mashariki na kusini mashariki ya Kobané-mkurugenzi wa shirika hilo la haki za binaadam la Syria Rami Abdel Rahmane ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.
Wanamgambo wasiopungua tisa wa IS wameuliwa,bomu lilipovurumishwa dhidi ya kifaru chao mashariki ya mji huo.Ingawa idadi yao ni ndogo na hawana silaha za kutosha,hata hivyo wapignaji wa kikurd wanapambana na wanamgambo wa itikadi kali wa IS wanaomiliki vifaru,silaha nzito nzito na makombora-shirika hilo la haki za binaadam linasema.
0 comments:
Post a Comment