Léonce Ngendakumana, mwenyekiti wa muungano wa upinzani nchini Burundi ADC-Ikibiri,
Esdras Ndikumana
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Burundi wa ADC
Ikibiri, Leonce Ngendakumana amehukumiwa kifungo cha mwaka moja jela.
Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa la AFP, leonce
Ngendakumana amesema anatuhumiwa kwa kosa la mashtaka ya uongo dhidi ya
chama tawala, na ameshutumu hukumu hiyo ambayo amesema ni ya kisiasa
inakuja wakati huu Burundi ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka
2015.
Ngendakumana amehukumiwa kwa ajili ya shutuma za uongo, kashfa
na chuki ya kikabila kutokana na yaliyomo katika barua iliyotumwa
Februari kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon,
ambamo alikituhumu chama tawala nchini Burundi, CNDD -FDD kuandaa mpango
kama ule uliondaliwa nchini Rwanda ambao mwisho wa siku uliishia
kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994.Leonce Ngendakumana ndiye kiongozi wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Burundi ADC/Ikibiri, mara kadhaa amekuwa akimemea serikali ya Burundi kutokana na kile anachodai hujma za serikali dhidi ya upinzani kwa kuwanyima haki ya kujieleza.
0 comments:
Post a Comment