Oct 1, 2014

Kesi ya kwanza ya Ebola yathibitishwa Marekani

Marekani imethibitisha kesi ya kwanza ya virusi vya Ebola nchini katika mji wa Dallas, ambayo pia ni ya kwanza nje ya bara la Afrika.
Kitengo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kimetangaza kwamba, mgonjwa wa kwanza aliyeambukizwa Ebola ni mwanamume na kwamba aligunduliwa jana Jumanne. 

Mkuu wa kitengo hicho Thomas Frieden amesema kuwa, mgonjwa huyo alianza kuumwa tangu alipokuwa nchini Liberia na kusafiri kuelekea jimbo la Texas, ambapo alipofika Marekani alilazwa hospitali na kuwekwa katika karantini baada ya kuonesha dalili za homa ya Ebola.

Wakati huo huo Pentangon imetangaza kuwa itapeleka askari 1,400 wa Marekani nchini Liberia ili eti kutekeleza ahadi yake ya kukabiliana na kuenea zaidi ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika. 

Tayari watu zaidi 3,000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo magharibi mwa Afrika.

0 comments:

Post a Comment