Sep 22, 2014

UMATADA KUPEWA ARDHI



 MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA MHE DR NAJIM AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO HAPO JANA.


Ahadi ya kuwapatia Ardhi ya kutosha Umoja wa Maendeleo Wakaazi wa Mkoa wa Tanga Waishio Dar es salaam (UMATADA) imetolewa.

Ahadi hiyo imetolewa jana katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Al haramaini iliyopo Ilala Jijini Dar es salaam

Akitoa ahadi hiyo Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Mhe Dr Najim amesema,”kuzungumzia heka hamsini kwa chama kikubwa kama hiki ni fedheha ni muhimu tuwe na heka elfu mbili”alisema kwa msisitizo mkubwa huku akishangiliwa na wajumbe

Aliendelea kusema kwamba “nimevutiwa na yaliomo katika risala yenu,kwa kuwa nami ni mwanachama na ni mdau wa maendeleo nina ahidi nitatumia kila njia kuhakikisha nawapatia ardhi yenye ukubwa wa heka elfu mbili na tutakapo kutana katika mkutano mkuu wa mwaka nitawafahamisha hatua nitakayofikia

Dr Najim ambaye pia ni  mkurugenzi wa madaini Tanzania alimwakilisha Mgeni Rasmi Diwani wa kata kwematiku Mhe Bereko.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wajumbe,Al haj Abdallah Sabaya alisema Umoja wao umebahatika kupata shamba katika kijiji cha Kwamsala lenye ukubwa wa heka Hamsini lakini wameshindwa kuliendeleza kutokana na mgogoro.

Kupitia risala hiyo aliutaja mgogoro huo kuwa ni madai ya kijiji cha komarasa kwamba shamba hilo lipo ndani ya mipaka ya kijiji chao na kumuomba Mhe Diwani aingilie kati mgogoro huo.

Aidha kupitia mkutano huo Umoja huo ulizundua Vitambulisho maalumu ambapo Mhe Dr Najim aliwakabidhi wanachama.

Umoja huo ulioanzishwa mwaka 1999 hadi sasa una wanachama zaidi ya 275.
 

 BAADHI YA WANACHAMA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MKUTANO HUO.

 
 VIONGOZI WA UMATADA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MWAKILISHI WA MGENI RASMI MHE DR NAJIM
 KATIBU WA SACCOS AKIWASILISHA TAARIFA ZA MAENDELEO YA SACCOS YA CHAMA HICHO.

 AL HAJ ABDUL SABAYA AKISOMA RISALA KWA NIABA YA WAJUMBE
 MHE DR NAJIM AKIMKABIDHI KITAMBULISHO MMOJA WA WANACHAMA WA UMATADA MUDA BAADA YA KUZINDUA VITAMBULISHO VYA UMATADA



0 comments:

Post a Comment