Sep 28, 2014

OIC: Viongozi wa Israel washtakiwe kwa kutenda jinai


 OIC: Viongozi wa Israel washtakiwe kwa kutenda jinai
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito wa kushtakiwa viongozi wa kijeshi na kisiasa wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu.
Iyad Amin al Madani Katibu Mkuu wa OIC ameikosoa Israel kwa kuwafanyia Wapalestina vitendo visivyo vya kibinadamu kwa miongo kadhaa sasa. 

Amesema kuwa, kuna kesi kubwa ya kuitaja Israel kuwa ni utawala wa ‘ubaguzi wa rangi’ ambao unapaswa kushughulikiwa kimataifa. 

Al Madani ameongeza kuwa, wamekuwa wakifanya majadiliano ya kuishauri serikali ya Palestina kujiunga na Mkataba unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kuwa mwanachama wa korti hiyo. 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia amesema, OIC inaunga mkono mpango wa Palestina wa kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liainishe muda wa kuondoka Israel katika ardhi inazozikalia kwa mabavu za Palestina.

0 comments:

Post a Comment