Sep 22, 2014

MAHUJAJI WA G8 WAASWA


MWENYEKITI WA TAASISI YA AL MADINA SHEIKH ALLY MUBARAKAH AKIONGEA KATIKA SEMINA ILIYOFANYIKA JANA KATIKA UKUMBI WA AL HARAMAIN JIJINI DAR ES SALAAM

Kundi la Mahujaji wapatao Mia sita linalo undwa kwa Ushirikiano wa Taasisi nane linalojulikana G8 wameaswa kutokujihusiha na mambo yatakayopelekea kuharibu Hijja zao.

Akizungumza katika Semina ya mwisho kwa Mahujaji wa taasisi hizo,Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Madina Sheikh Ally Mubarakah amesema ni vyema kwa Mahujaji wakifika katika viwanja vitukufu kufanya ibada pekee kwani ndicho walicho kisumbukia.

Aliwaasa mahujaji kwamba wasiwe na tabia ya kudadisi au kusema juu ya tofauti ya huduma baina ya kundi na kundi.

“Ndugu zangu mahujaji watarajiwa,kwa uwezio wa Allah tuna kwenda Makkah basi tujiepushe na mambo ambayo hayana msingi wala faida”alisema

Aliendelea kusema kwamba “utakuta watu wanasema kundi au taasisi Fulani imekula chakula kizuri au imelala hotel mzuri,ndugu zangu haya siyo yaliyotupeleka”

Semina hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Al haramain uliopo Jijini Dar e salaam.

G8 inaundwa na Taasisi za Al madina,Ummul Quraa,Tabazat Baabu salaam,Markaz Shamsiyyah,Ahlul Baytu,East Afrika Hajj Trust,Islamic  Development Centre na Daarul Hadiith.

G8 Litaondoka tarehe 23,24 na 26 mwezi huu In Shaa Allah.

Munira blog inawatakia safari njema na HIJJA MABROUL

 NAIBU KADHI MKUU WA TANZANIA AL HAJ SHEIKH ABOUBAKRI ZUBEIR AKIZUNGUMZA KATIKA SEMINA HIYO.



BAADHI YA MAHUJAJI WAKIWA KATIKA SEMINA YA MWISHO ILIYOFANYIKA JANA

0 comments:

Post a Comment