Sep 28, 2014

Libya yaomba kusaidiwa kupambana tishio la ugaidi

Libya imeitaka jamii ya kimataifa iisaidie silaha zaidi, kurejesha amani nchini na kuhuisha tena taasisi zake au iamue kutangaza kwamba nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika inapaswa kukabiliana na ugaidi yenyewe.
Hayo yamesemwa na Aguila Saleh Lissa Spika wa Bunge wa Wawakilishi la Libya katika hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.  

Ameongeza kuwa, iwapo jamii ya kimataifa ingeuzingatia mgogoro wa nchi yake tangu mwanzo hali isingekuwa kama ilivyo sasa.
 
 Serikali ya Tripoli imeshindwa kudhibiti makundi yenye silaha yaliyosaidia kuangushwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi, ambayo kwa sasa yanapigana yenyewe kwa yenyewe. 

Kundi moja la wanamgambo linalopinga serikali kutoka mji wa Misrata mwezi Julai lilidhibiti mji mkuu Tripoli na kulazimisha Bunge kuhamia katika mji wa mashariki wa Tobruk. 

Mwenyekiti wa Bunge la Wawakilishi la Libya amesema, haikubaliki kufumbia jicho ugaidi nchini Libya na kwamba kushindwa kulisaidia jeshi silaha na mafunzo ili kufanikisha vita dhidi ya ugaidi, ni kwa manufaa ya makundi yenye kufurutu ada.

0 comments:

Post a Comment