Sep 30, 2014

Marekani yalenga viwanda vya gesi vya Syria

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa jana na Marekani kwa madai ya kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri  la DAESH yamevilenga viwanda vya gesi huko mashariki mwa Syria.

Rami Abdul-Rahman, mkuu wa ofisi ya haki za binaadamu nchini Syria, amethibitisha habari hiyo huku akihoji malengo ya mashambulizi hayo. 

 Duru za habari zinasema, viongozi wa kundi la Daesh wamekuwa wakitoa indhari kwa wanachama wake kuondoka katika maeneo ambayo yanakusudiwa kulengwa na ndege za Marekani, suala ambalo limewatia shaka weledi wengi wa mambo juu ya azma ya Washington katika mashambulizi hayo. 

 Mashambulizi hayo ya Marekani yamekilenga pia kiwanda cha kusafishia mafuta ambacho kilikuwa kikidhibitiwa na wanachama hao wa Daesh, kwa madai ya kuwadhoofisha kiuchumi, suala ambalo hata hivyo linatajwa kuathiri uchumi wa taifa la Syria, hasa kwa kuzingatia kuwa, kabla ya kutekelezwa mashambulizi hayo, wanachama wa Daesh wanakuwa tayari wameondoka eneo husika na hivyo kuharibu tu miundombinu na kuua raia pekee. 

Mkuu wa kituo cha haki za binaadamu nchini Syria, amesema kuwa mashambulizi mengi ya Washington katika maeneo yanayodhitiwa na Daesh yanaishia kuharibu miundombinu ya taifa hilo

0 comments:

Post a Comment