Sep 30, 2014

Waislamu Ufaransa waandamana kupinga Daesh

Waislamu nchini Ufaransa wamefanya maandamano kulaani jinai za kutisha zinazofanywa na kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq na Syria.

Hayo ni maandamano ya tatu kufanyika mjini Paris, Ufaransa kupinga kundi hilo la kigaidi. Waislamu hao wa Ufaransa pia wamelaani mauaji ya raia wa nchi hiyo aliyeuawa siku tatu zilizopita na wanachama wa kundi hilo huko Algeria. 

Herve Gourdel aliuawa na wanachama wa kundi linalojiita ‘Jundul-Khilaafah’ ambalo ni sehemu ya kundi la Daesh, baada ya magaidi hao kutoa onyo kwa serikali ya Ufaransa iache kuingilia kijeshi nchini Iraq.

Hii ni baada ya Rais François Hollande wa Ufaransa kutangaza siku chache zilizopita kwamba nchi hiyo imeanza mashambulizi dhidi ya kundi la Daesh nchini Iraq. 

Waandamanaji hao pia wamelaani fikra na itikadi potofu za kundi hilo la Daesh na kuwataka Waislamu wengine duniani kujitenga nalo.

0 comments:

Post a Comment