Na Khamis Haji, Istanbul
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad amesema hali ya amani na utulivu katika eneo la Afrika
Mashariki ni ya kuridhisha na wawekezaji vitegauchumi pamoja na wafanyabiashara
wanaotaka kutumia fursa zilizopo katika eneo hilo waje na waondowe hofu.
Maalim Seif ameyasema hayo katika mkutano wa Uchumi
wa Dunia (WEF) unaoendelea katika jiji la Istanbul nchini Uturuki alipotakiwa
kutoa maoni yake juu ya hali ya usalama katika eneo hilo la Afrika Mashariki.
Amesema iliwahi kujitokeza hali ya kukithiri vitendo
vya kiharamia vilivyo sababishwa na kukosekana utulivu katika nchi ya Somalia,
lakini matukio hayo hivi sasa yamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mashirikiano
ya pamoja kati ya nchi zilizopo jirani pamoja na Jumuiya ya Kimataifa.
Amesema nguvu hizo za jumuiya ya kimataifa zinapaswa
kuendelezwa, ikiwemo kuzijengea uwezo nchi za Afrika katika kukuza upatikanaji
wa ajira kwa vijana, ili kuwaepusha na uwezekano wa kushawishiwa na makundi ya
watu waovu ambayo yamekuwa chanzo cha kuongezeka matendo maovu.
“Hali katika eneo la Afrika Mashariki ni salama sana
kuna vivutio vya kila aina, wawekezaji
tumieni fursa hii kuja kufungua miradi yenu”, amesema Maalim Seif.
Amesema ni jukumu la Jumuiya ya Kimataifa kuzipa
msukumo nchi zenye matatizo ya uchumi, likiwemo tatizo kubwa la uhaba wa ajira
miongoni mwa vijana, ambalo litawaepusha vijana na tabia ya kurubuniwa kuingia katika matendo
yasiofaa.
Maalim Seif Ahudhuriwa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Uturuki.
- Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akijiandaa kuhutubia mkutano wa Dunia wa Uchumi, ambapo amezilaumu baadhi ya nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani kutokana na sera zao nchini Irak na Syria.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar wa Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad akiwa na Waziri Mkuu wa Mali, Mhe. Moussa Mara (kulia) na
viongozi wengine wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Uchumi wa Dunia, jijini
Istanbul, Uturuki.
Mh. Maalim Seif akibadilishana mawazo na Afisa
katika Serikali ya Uturuki wakati wa mkutano wa Uchumi wa Dunia (WEF).
Mhe.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,akizungumza na
Balozi wa Tanzania nchini Italia, ambaye pia anahusika na Uturuki, James
Msekela wakati wa mkutano mkuu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim
Seif akitoka kwenye mkutano wa WEF. Kushoto kwake askari wa Uturuki
akimhakikishia ulinzi.
Wataalamu mbali mbali katika masuala ya Ubunifu
na Ujasiri Amali, wakiwemo kutoka Israel, Marekani na Ujerumani waliofika
katika mkutano wa WEF baada ya kuwasilisha mada zao. Mjadala wa mada hizo
ulimhusisha Mhe. Maalim Seif.
0 comments:
Post a Comment