Sep 28, 2014

Hukumu dhidi ya wafuasi wa Ikhwan yaakhirishwa

Mahakama ya Misri imeakhirisha hukumu dhidi ya wafuasi 8 wa Ikhawanul Muslimin wanaodaiwa kuwa walishiriki maandamano ya kupinga serikali kinyume cha sheria.
Hukumu dhidi ya wafuasi hao wa Ikhanul Muslimin imeakhirishwa hadi Mahakama Kuu itakapoamua uhalali wa sheria ya kupinga maandamano kwa mujibu wa katiba. 

Wakati huo huo baadhi ya wanasheria wa Misri wamefungua mashtaka kupinga baadhi ya vipengee vya sheria hiyo, wakisema kuwa vinakinzana na haki ya kujieleza ya waandamanaji wakati katiba tangu mwanzo inatoa haki hiyo.

 Katika upande mwingine mahakama ya Misri imeakhirisha hukumu ya mwisho ya kesi mpya inayomkabili dikteta aliyepinduliwa nchini humo Hosni Mubarak.  

Mahakama hiyo tarehe 2 Juni 20012 iliwahi kumhukumu Hosni Mubarak adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kwa kushiriki kwenye mpango wa kuwauwa waandamanaji katika ghasia zilizotokea tarehe 25 Januari mwaka 2011. 

Hata hivyo, kesi hiyo iliamuliwa kusikilizwa upya baada ya Hosni Mubarak kukata rufaa.

0 comments:

Post a Comment