Apr 23, 2014

MAJAMBAZI YAKAMATWA


Majamabazi walionaswa wakiwa na bunduki aina ya SMG  haipo pichani wakishushwa kutoka katika gali chini ya ulinzi wa askali kanzu waliopo pembeni mwao.

Mkuu wa Kituo kidogo cha Matemanga F 1678 Cpl. Gwalugano kwa kushirikioana na asikali polisi wenzake watano wamewakata Majambazi wawili wakiwa na Bunduki aina ya SMG ambayo hadi sasa namba zake bado hazijafahamika.

Aidha katika tukio hilo pia watuhumiwa hao walinaswa wakiwa na Risasi 19 magazini  ndani ya, Vifaa viwili vya kuficha sura (Maski) pamoja na Vifaa mbalimbali na silaha za kijadi vilivyo ashilia kuwa maharamia hao walijiandaa kwenda kufanya tukio la kinyama.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamukia April 11, 2014 katika Kijiji cha Kiuma nje kidogo ya Kituo hicho kilichopo katika Tarafa ya Matemanga Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma ambapo pamoja na kukutwa na vifaa hivyo majambazi hao pia walikutwa waikiwa na Mapanga mawili,makoti mazito mawili na Tochi moja ya kujifunga kichwani.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Akili Mpwapwa amewataja majambazi hao kuwa ni  Rashid Anafi (34) na Akimu Jafari (32) Wayao wakazi wa Mtaa wa Ruvuma Mjini Songea.

Kamanda Mpwapwa aliendelea kufafanua kuwa Majambazi hao walinaswa kufutia taarifa zilizotolewa na wasamalia wema na kwamba katika tukio hilo watuhumiwa hao walinaswa wakiwa wanasafiri kutoka Mjini Songea
kuelekea mjini Tunduru kwa kutumia pikipiki aina ya Snlg yenye namba za usajiri T 725 Cpu.

Alisema kufuatia hali hiyo watuhumiwa hao watahamishwa katika kituo kikubwa cha Polisi cha Wilaya yaTunduru kwa ajili ya mahojiano zaidi na baadae kufikishwa Mahakamani ili sheria iweze kufuata mkondo wake kuanzia wiki ijayo.

Pamoja na kuwapongeza wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa maharamia hao pia ametoa wito kwa wananchi kuendele kutoa ushirikianao kwa jeshi
la polisi ili kudhibiti matukio ya uhalifu ambayo yanaweza kusababisha madhara miongoni mwao.

0 comments:

Post a Comment