Jan 13, 2014

Wananchi wa Libya waandamana kupinga machafuko

Wakazi wa mji wa Benghazi nchini Libya wamefanya maandamano makubwa wakipinga machafuko, ukatili ma mauaji yanayoendela kufanyika katika mji huo wa mashariki mwa Libya.

Waandamanaji hao wamelaani pia vitendo vya kutekwa nyara raia, na ukosefu wa amani na wameitaka serikali ya Tripoli kufanya jitihada kubwa za kulinda usalama wa raia.
Mji wa Benghazi ambao ndiyo kitovu cha mapinduzi ya wananchi wa Libya yaliyomuondoa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gadafi tarehe 17 Februari mwaka 2011 kwa muda sasa umekumbwa na machafuko na mauaji yanayowalenga raia na askari na vilevile utekaji nyara.

Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa zaidi ya watu 200 wameuawa katika machafuko ya sasa ya Benghazi wengi wao wakiwa shakhsia wa kisiasa, wanajeshi na wasomi.

0 comments:

Post a Comment