Jan 13, 2014

Al-Majid azikwa na ndugu wa Osama nchini Saudia

Mazishi ya Majid al Majid, gaidi aliyekuwa na uhusiano na mtandao wa al Qaida aliyefariki dunia hivi karibuni nchini Lebanon, yalifanyika siku ya Jumamosi usiku baada ya sala ya Isha mjini Riyadh, Saudia. 

Kwa mujibu wa duru za habari idadi ya watu kadhaa wakiwemo ndugu wa kiongozi wa zamani wa kundi hilo la kigaidi la Al-Qaida walishiriki mazishi hayo kutokana na kuwepo udugu wa kifamilia kati ya al-Majid na Osama bin Laden. 

Aidha habari zinasema kuwa, familia ya gaidi huyo anayetajwa kuwa na ripoti nyingi za kigaidi duniani, imeahidi kulipiza kwa kile ilichosema kuwa eti ni ulipizaji kisasi kwa mauaji ya ndugu yao huyo. 

 Al-Majid alifariki duania akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la Lebanon kufuatia kuzorota kiafya hali yake. Hata hivyo kuna wasiwasi kuhusiana na kifo cha gaidi huyo, hasa kwa kuzingatia kuwa, kundi lake la kigaidi linalojiita Brigedi ya Abdullah Azzam lenye mafungamano na kundi la Al-Qaida, linatuhumiwa kwa kuhusika na vitendo kadhaa vya kigaidi ukiwemo mripuko wa karibu na ubalozi wa Iran mjini Bairut, Lebanon. 

 Aidha weledi wa mambo wanakitaja kifo cha al-Majid kuwa, kilichotekelezwa kwa lengo la kuficha ushahidi wa mahusiano ya karibu kati yake na Bandar bin Sultan, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia.

0 comments:

Post a Comment