Jan 13, 2014

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yaadhimisha miaka 50 ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar.



Miaka 50 ya mapinduzi ya ZanzibarMiaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar



Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hii jana inaadhimisha kumbukumbu ya miaka hamsini ya mapinduzi tukufu yaliyomaliza utawala wa Kisultani visiwani humo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ataongoza sherehe hizo ambazo pia zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania bara akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal.

Marais mbali mbali pia wanahudhuria sherehe hizo akiwemo rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Rais Shein amewataka wananchi kushiriki kikamilifu na kuonesha umoja na mshikamano walionao katika sherehe hizo za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Karume.

0 comments:

Post a Comment