Jan 11, 2014

.....PAMOJA NA HAYO,LAKINI HUU NI UKATIRI UNAOSTAHILI KUPINGWA.


 Munira blog inawaomba radhi wasomaji wake kwa picha hizi,lakini tunaziweka picha hizi kwa shingo upande tukiitaka jamii kuunga nguvu za pamoja kuhakikisha tunapinga ukatiri huu kwa nguvu zote.

Kwani licha ya kuwa ni mwizi au jambazi,lakini tukumbuke ya kwamba huyu ni bin adamu ambaye ana haki ya kuishi.

Pamoja na hayo vipo vyombo vyenye mamlaka ya kutoa adhabu.
 


WANANCHI wenye hasira wa Kijiji cha Kisiwa Kata ya Kiloka Wilaya ya Morogoro Vijini jana usiku wamewauwa kisha kuwachoma moto watu watu  wanaosadikiwa kuwa majambazi.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo Bw Shabani Mango alisema majambazi hao walivunja nyumba ya mkazi mmoja wa kijijini hicho na kuiba shilingi  490,000
 
"Jamaa walifka hapa majira ya saa 8 usiku wakiwa na pikipiki Feko yenye namba za usajiri T310 BTC wakipakizana mshikaki,walivunja geti na kuingia ndani ambapo walipora kiasi hicho cha fedha "alisema Mango na kuongeza" 
 
Fedha hizo Mwalimu Said Swale Tajiri alizikopa jana mchana kwenye saccos ya Moboto kwa lengo la kumlipia ada mdogo wake anayesoma jijini Dar es salaam.
 
Mwenyewe alipanga leo ijumaa (jana) kwenda Dar kulipa ada nahisi jamaa walipata taarifa kwamba Ticha ana mzigo ndani"alisema Bw Mango.

Kwa upande wake afisa mmoja wa jeshi la polisi alithibitissha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majambazi hao kuwa ni Emmanuel Mlapoli na Kessy Benno ambaye ni boda boda naye pack Pangawe jeshini.
 
''Jambazi mmoja jina lake bado halijafahamika na kwamba eneo la tukio tulikuta pikipiki aina ya Feko yenye namba za usajiri T 3710 BTC mali ya marehemu Kessy Benno ambaye ni makzi wa Kingulwila stesheni manispaa ya Morogoro'alisema Afande huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwakuwa sio msemaji wa jeshi hilo. 

KWA HISANI YA MATUKIO NA MICHAPO.

0 comments:

Post a Comment