Hazem Beblawi
Waziri Mkuu wa Mpito wa Misri
ameambia BBC kuwa wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood wanaweza
kushiriki Uchaguzi Mkuu ikiwa watalaani ghasia na machafuko.
Lakini vugu vugu la Muslim Brotherhood, ambalo liliorodheshwa kuwa kundi la kigaidi hivi karibuni, limekanusha madai ya kuhusika na ghasia zinazokumba Misri.
Chama hicho cha Muslim Brotherhood, kiliongoza serikali ya kwanza kuwahi kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia nchini Misri, ambayo iliondolewa madarakani miezi sita iliyopita na jeshi.
Kiongozi wake Mohammed Morsi anakabiliwa na mashitaka kadhaa ya uhalifu.
0 comments:
Post a Comment