Jan 24, 2014

Chikawe: Kipaumbele ni kufumua jeshi la polisi



Waziri mpya wa Mambo ya Ndani, Mathius Chikawe amesema kuwa, moja ya mambo atakayoyapa kipaumbele katika fremu ya kuimarisha usalama ni kulifanyia marekebisho makubwa jeshi la polisi. 

 Waziri Chikawe alisema hayo alipokutana na maafisa wa ngazi za juu wa polisi akiwemo Inspekta Mkuu, Ernest Mangu.
Waziri mpya wa Mambo ya Ndani wa Tanzania amesema miongoni mwa uozo anaotarajia kukabiliana nao katika jeshi la polisi ni ulaji rushwa. 

Amesema tatizo hilo ni moja ya mambo makuu yanayochangia vyombo vya usalama kulegalega na matokeo yake ni kuongezeka visa vya ukosefu wa usalama nchini Tanzania.

Mathias Chikawe alihamishwa kutoka Wizara ya Sheria hadi ile ya Mambo ya Ndani kufuatia mabadiliko yaliyofanyika katika baraza la mawaziri la Tanzania wiki iliyopita. 

Kabla ya mabadiliko hayo, Wizara ya Mambo ya Ndani ilikuwa ikiongozwa na Dkt. Emanuel Nchimbi.

0 comments:

Post a Comment