Jan 14, 2014

KUMBUKUMBU YA KUZALIWA MTUME S,A,W ZAFANA


 Muhammad
Sherehe za kumbukumbu za kuzaliwa Mtume Muhammad (S A W) zilizo fanyika jana katika viwanja mbalimbali zilifana.

Kwa mujibu wa waandishi wetu waliohudhuria katika maeneo mbalimbali walishuhudia mamia ya Waislamu wakiungana na waislamu wenzao duniani kusherehekea maulidi hayo.

katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es alaam yalifanyika maulid ya mkoa ambapo yalipambwa kwa mambo mbalimbali yenye kuvutia.


Waandishi wetu walishuhudia zafa (maandamano ya amani ya kiislamu) majira ya jioni yakipita katika barabara za katikati ya jiji huku yakionekana kuratibiwa vizuri.

Viongozi mbalimbali waliopata fursa ya kuongea walihimiza amani,mshikamano na umuhuimu wa kutafuta elimu.

Aidha waandishi wetu kutoka maeneo ya Tanga,Bagamoyo,Zanzibar na Lindi wameripoti juu ya kufana kwa maaulidi hayo yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

kitaifa maulid hayo yalifanyika mkoani Kigoma.

 

0 comments:

Post a Comment