Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan
Kusini wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbia vita
vinavyoendelea katika mji wa Malakal.
Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu wengi kupindukia. Watu hao walikuwa wanatoroka vita vinavyotokota katika mji wa Malakal.
Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar, kwa kuwa na njama ya kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo.
0 comments:
Post a Comment