Jan 13, 2014

HASHIM SAGAFF AFARIKI

Aliyekuwa mbunge wa Dodoma Hashim Sagaf amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia mapema leo hii ni kwamba Hashim Sagaf amefariki leo Asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

"Tutamswalia katika msikiti wa Bungoni uliopo ilala na tutamzika leo saa kumi katika makaburi ya kisutu"kilisema chanzo chetu.

Katika enzi za uhai wake bwana Sagaff aliwahi kushika nyadhifa kadhaa ikiwemo nafasi ya ubunge na kuwa ni mmoja viaongozi katika taasisi ya DYCCC.

INNAA LILLAAH WAINNAA ILAYHI RAJIUN

0 comments:

Post a Comment