Dec 21, 2013

UFAHAMU UNYAMA ULIOFANYWA KATIKA OPARASHENI YA TOKOMEZA UJANGILI

Ifuatayo ni sehemu ndogo sana ya unyama uliofanywa na askari katika oparesheni ya tokomeza ujangili kama ina vyoelezwa na mwenyekiti wa kamati mhe limbeni.

Lembeli alisema ulibainika unyama mkubwa ikiwemo viongozi, madiwani, wenyeviti wa vijiji na vitongoji na watumishi wa serikali walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza.

“Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao,” alisema.


Alisema Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume akishuhudia.

“Pia alidai kulazimishwa kuchora picha ya chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake. 

Vilevile, Neema Moses wa Babati alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa afanye mapenzi na wakwe zake na pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.

“Baadhi ya akina mama walidai kubakwa na kulawitiwa. 
Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na askari wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku.

“Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu wa Operesheni Tokomeza Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki,” alisema.
 
Alibainisha kuwa baadhi ya watuhumiwa waliopelekwa katika kambi za mahojiano walidai kuteswa na kupewa adhabu zinazokiuka haki za binadamu ikiwemo kuvuliwa nguo zote.

“Mfano Diwani wa Kata ya Sakasaka Wilaya ya Meatu, Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti,” alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na ukatili mkubwa, baadhi ya kambi za mahojiano zilipewa majina ya Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro), Duma na Andajega (Serengeti).

Aliongeza kuwa pia operesheni hiyo iliongozwa kwa rushwa ambako wananchi walidai kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwa watumishi wanaosimamia mapori ya akiba ya Maswa, Kigosi, Moyowosi, Burigi, Kimisi na Mkungunero.

0 comments:

Post a Comment