Imeelezwa kwamba Uislamu haukubaliani na msimamo mkali.
Hayo yapo katika khutuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Semina hiyo ilifanyika katika kituo cha kiislamu cha kimisri kilichopo Chang'ombe Jijini Dar es salaam.
Akiwahutubia maimamu,waalimu na makhatwib waliohudhuria semina hiyo,mkuu wa kituo hicho Dr Osama Bin Mahmuod Bin Ismail amesema Uislamu ni dini ya amani na ni dini ya kukimbiliwa na kamwe si dini ya kukimbiwa.
Akinukuu aya kadhaa ndani ya Qur aan,Dr Osama alisema Uislamu unakataza kulazimsha au kutumia msimamo mkali,kwani kufanya hivyo ni kinyume cha mafundisho sahihi ya Allah S,W na Mtume wake Muhammad S,A,W.
Ndugu wana semina,Allah ana mwambia Mtume wake Muhammad S,A,W kwamba kwa hakika tumekiteremsha kitabu (Qur aan) kwa haki,ili uwahukumu watu kupitia kitabu hicho,sasa ifahamike katika watu hao,wengine siyo Waislamu"alisema.
Aidha alikitaja kiswa cha bedui mmoja aliyekojoa ndani ya msikiti na maswahaba walipo taka kumuadhibu Mtume S,A,W,aliwakataza,alisema hii ni sehemu ya mafunzo yanayo onesha Uislamu unapinga jazba,kutumia nguvu na msimamo mkali.
"Ndugu zangu mwalimu ni Twabibu wa umma,hivyo basi muna jukumu la kuwafahamisha watu usahihi wa Uislamu,hekima na busara zina nafasi kubwa katika kulingania kuliko nguvu na Jazba",mwisho wa kumnukuu.
Katika semina hiyo,masheikh mbalimbali walipata fursa ya kuzungumza akiwemo Sheikh Suleiman Kilemile,Naibu Mufti Sheikh Ally Mkoyogole,Sheikh Rashid Mziwanda na Sheikh Ally mbwera huku kauli mbiu ya semina hiyo ikiwa ni UISLAMU UNAPINGA MSIMAMO MKALI.
Oct 28, 2013
UISLAMU Unapinga Msimamo Mkali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment