Oct 28, 2013

Ukubwa wa Gharama za matibabu ya Saratani ni Kikwazo.

MWENYEKITI Mtendaji wa kampuni za IPP, Reginard Mengi, amesema asilimia 10 ya wanawake wenye ugonjwa wa saratani ya matiti  ndio wanaofika hospitali kupatiwa matibabu huku wengine wakishindwa kwenda kwa kukosa fedha.

Mengi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana katika matembezi ya hisani yaliyofanyika katika viwanja vya  Hospitali Ocean  Road  ambapo lengo lilikuwa kukusanya sh milioni 100 kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wa saratani ya matiti nchini.

Alisema lengo lao limefanikiwa kutokana na wahisani mbalimbali kuchangisha fedha hizo.

Alisema watu wengi  wamefariki kutokana na kushindwa kulipia fedha za matibabu ya ugonjwa huo na wengi walibaki  nyumbani kwa kuona aibu.

Alisema fedha hizo zitawasaidia wagonjwa hao kwa kiasi kikubwa na kuwapa elimu.

Alisema ili kuuepuka ugonjwa huo kuna haja ya kufanya mazoezi, kula mboga za majani na matunda kwa wingi pia kuepuka kula vyakula vya mafuta na nyama nyekundu.

Pia alisema matumizi ya tumbaku yakiachwa yatasaidia kufanya afya bora na uwezekano wa kupata saratani ya aina yoyote kupungua.

Mmoja wa wagonjwa wa saratani, Asha Kunti, ambaye ni mwalimu kutoka Shule ya Msingi Ipagala Dodoma alisema ugonjwa wa saratani ya titi ulianza kumsumbua mwaka 1969.

Alisema baada ya kupatwa na ugonjwa huo alilazimika kwenda Dar es Salam kupatiwa matibabu.

1 comments:

  1. niligunduliwa na saratani mnamo 2019 na nimekuwa nikitafuta tiba tangu wakati huo. Oktoba mwaka jana nilipokaribia kukata tamaa, nilikutana na chapisho kwenye mtandao ambapo nilinakili barua pepe ya mwanamume anayeitwa dr DAWN inayotoa suluhisho la mitishamba kwa magonjwa. niliwasiliana naye na kupata maelewano naye akanitumia dawa ya mitishamba kupitia united parcel service pamoja na maelekezo ya jinsi ya kuitumia. kwa mshangao wangu mkubwa, nilipona baada ya siku 14 za kutumia dawa kama alivyohakikishiwa na daktari.
    Niliamua kushiriki hii kwa sababu najua kuwa kuna watu wengi huko ambao wanahitaji msaada. au umtumie ujumbe kwa WhatsApp.+2349046229159 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    Anaweza pia kuponya magonjwa mengi kama hayo

    {1}VVU na UKIMWI

    {2}Kisukari

    {3}Kifafa

    {4} Saratani ya Damu

    {5} HPV

    {6} ALS

    ReplyDelete