Sep 21, 2013

WAZAZI TURATIBU MUDA WA WATOTO WETU-WITO



ALIYEJISHIKA SHAVU NI MWENYEKITI BODI SHULE YA DYCCC HASSAN AKRAB,KULIA KWAKE NI MWALIMU MKUU WA SHULE HIYO KHALID HEMED NA WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI SHEIKH OMAR AWADH AMBAYE NI KATIBU MKUU


HUYU NI MZAZI WA MALIYAT HAIDAR KASSIM AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI



HAWA NI SEHEMU YA WAHITIMU WASICHANA


MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA DYCCC HASSAN AKRAB AKITETA JAMBO NA KATIBU WA BODI HIYO SHEIKH OMAR AWADH

MADAM LEILA DHIYEB (AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA MWALIMU MKUU WA KWANZA WA WAKHITIMU HAWA WAKATI HUO WAKIWA DARASA LA KWANZA) PAMOJA NA MWENYEKITI WA BODI HASSAN AKRAB WAKIWAKABIDHI TUZO BAADHI YA WAKHITIMU NA WASHINDI WA MASOMO MBALIMBALI LEO HII.


BAADHI YA WAZAZI WA KIUME WAKIWA KATIKA MAHAFALI HAYO.


BAADHI YA WAZAZI WA KIKE WALIOHUDHURIA MAHAFALI HAYO.

Wito umetolewa kwa wazazi nchini kuratibu muda wa watoto wao kuangalia TV na Internet kwani ni sehemu ya kikwazo cha kufanya vizuri katika masomo yao mbalimbali.

Hayo yamesemwa hivi punde na Mgeni rasmi mzazi wa Maliyat Haidar Kassim katika Mahafali ya kuwaaga na kuwapongeza wanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya DYCCC YEMEN ENGLISH MEDIUM SCHOOL iliyopo Chang'ombe Jijini Dar es salaam.

Amesema moja ya siri za mafanikio ya mwanawe kufanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza (kwa kuwa na alama 1603 katika masomo sita yaliyofanyiwa mtihani shuleni hapo) ni wao wazazi kuratibu muda wa mtoto wao,kwani bila ya kuwaratibia muda watoto wetu wanatumia muda mwingi kwa kuangalia Tv na mambo ya Internet.

Akiendelea kutoa siri ya mafanikio kwa mtoto wake alisema,"Ni lazima wazazi watenge muda kupitia masomo ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kuhakiki kazi wanazopewa shuleni pamoja na kusikiliza maoni yao,"

Aidha alisema "wazazi wengi hawajafahamu umuhimu wa kuwapeleka watoto madrasa kusoma Qur aan,unapompeleka mtoto madrasa kwa wakati muwafaka (kuanzia miaka mitatu),mtoto anakuwa na uwezo mkubwa sana wa kumudu masomo mbalimbali,sasa hili tulipe kipaumbele,lakini pamoja na hilo basi liende sambamba na kuwalipa Ada waalimu wa madrasa ambao kimsingi wengi wetu hatuwatendei haki,kwa hakika inasikitisha sana kuona ada ya walimu wa madrasa ni ndogo mno na haitolewi kwa wakati,basi ni fursa mzuri kwa wazazi mbali ya kutoa ada lakini pia watowe swadaqa kwa walimu hao"mwisho wa kumnukuu.

Akisema kwa umakini mkubwa,mzazi wa Maliyat alikhitimisha kwa kusema ,'kimazingira,kwa hali ya kidunia ilivyo,ni sawasawa na kusema bahari imechafuka,sasa chombo pekee cha kuwavusha salama watoto wetu ni kuwapatia elimu bora na maadili mema"

Heshima ya mama Maliyat Haidar Kassim kuwa ni mmoja wageni rasmi imetokana na makubaliano ya busara ya Bodi ya shule hiyo kwamba wanafunzi watakao shika nafasi mbili za juu wazazi wao ndiyo watakao kuwa wageni rasmi. 

Katika mahafali hayo ya wanafunzi wanaokhitimu darasa la saba shuleni hapo,wanafunzi hao walionyesha umahiri mkubwa katika masomo mbalimbali ikwemo masomo ya sayansi,tehama,hesabu,michezo n.k kiasi cha kuwavutia wazazi waliohdhuria.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa  Shule hiyo Khalid Hemed akiwahutubia wanafunzi na wazazi katika mahafali hayo amesema "licha ya shule yetu kukabiliwa na changamoto kadhaa,bado shule yetu inafanya vizuri na kutokana mikakati tuliyojiwekea tunaamini shule yetu itakuwa ni miongoni mwa shule bora nchini Tanzania".



 KUTOKA KULIA NI MWENYEKITI BA BODI YA SHULE YA DYCCC HASSAN AKRAB,ANAYEFUATIA NI KATIBU WA BODI YA SHULE HIYI SHEIKH OMAR AWADH NA MWENGINE NI MZAZI WAKIBADILISHANA MAWAZO


MR KHALID HEMED,MWALIMU MKUU WA SHULE YA DYCCC YEMEN ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL WAKATI ALIPOKUWA ANAONGEA KATIKA MAHAFALI HAYO LEO HII.


MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA DYCCC HASSAN AKRAB AKIWA NA MWALIMU MKUU WA DARASA LA KWANZA AMBAO LEO NDIYO WAKHITIMU WA DARASA LA SABA MADAM LEILA DHIYEB WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

HONGERA MWANANGU NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA MGENI RASMI.



1 comments:

  1. ASALAM ALAYKUM WWB. MIE NIMEPENDEZWA SANA NA HARAKATI ZENU ZA KUWALEA WATOTO WA KIISLAM KATIKA MAADILI YANAYOTAKIWA

    ReplyDelete