Sep 21, 2013

Wapinzani kumwaga mboga leo




Vyama vitatu vya upinzani nchini Tanzania (CHADEMA,CUF na NCCR-MAGEUZI) Leo vinaanza safari yao ya kuwahamasisha wananchi kupinga marekebisho ya muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi uliopitishwa hivi karibuni bungeni Dodoma.

mkutano huo mkubwa utafanyika leo katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam.

Katika mkutano huo viongozi wakuu wa kitaifa wa vyama hivyo vitatu watazungumza na wananchi wanaotarajiwa kuhudhuria kwa wingi.

Awali viongozi hao walipanga mkutano huo utanguliwe na maandamano makubwa lakini kamanda wa jeshi la polisi nchi tanzania said mwema amezuwia maandamano hayo baada ya jana kufanya mazungumzo kwa masaa matatu na viongozi hao ambao kimsingi walikubaliana.

Munirablog ilipita katika viwanja vya jangwani asubuhi hii na kukuta yakifanyika maandalizi ya mwisho ambapo jukwaa kuu limewekwa maeneo ya mashariki wakati kla baada ya mita chache kuna bendera tatu za vyama vya Chadema,Cuf na NCCRA MAGEUZI zikiwa zimesimamishwa kwa pamoja.



 





0 comments:

Post a Comment