Sep 21, 2013

Tunahitaji KATIBA yenye Maslahi Kwa Wananchi-Prof Lipumba



 MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AKIONGEA KWA NIABA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI

Hatimaye viongozi wakuu wa vyama vya upinzani nchini wameweka bayana kwa kusema wanacho pigania ni kupata katiba itakayo hakikisha mali asili na rasilmali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote na siyo katiba yenye maslahi kwa mafisadi na mchwa wa hapa nchini.
Hayo yamesemwa jioni hii na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Haroun Lipumba kwa niaba ya vyama vya upinzani alipokuwa anazungumza na maelfu ya wananchi waliofurika katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam.

Amesema kilichotokea bungeni ni uchakachuaji wa marekebisho ya muswada wa katiba uliofanywa na wabunge wa CCM,kitu ambacho hatutokubali kwa gharama yoyote.

Ndiyo maana chama cha wananchi CUF kwa kuwa kinasimamia na kuunga mkono haki hakitosita kuunga mkono harakati zozote za kupigania haki iwe kwa taasisi au kwa chama chochote cha siasa,alisema.

"Ndugu zangu kwa muda mrefu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa aiiheshimu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,imekuwa inaiburuza tu,sasa sisi hatuwezi kuendelea kuliacha jambo hili liendelee ukizingatia Zanzibar ni taifa kamili"

Aliendelea kusema "Vijana wetu muanze kufanya mazoezi kwani suala la kudai katiba mpya na tume huru tutaliendeleza kwa gharama yoyote"Mwisho wa kumnukuu,kauli ambayo iliibuwa mayowe ya kushangiliwa na maelfu ya watu waliofurika viwanjani hapo.

kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI Mhe James Mbatia amesema Watawala wa Tanzania wanapaswa wafahamu kwamba katiba ni tendo la maridhiano,haihitajiki kutumia mabavu kama walivyofanya bungeni hivi karibuni.

'Tusisubiri watu wafe ndipo tukae mezani,tujifunze kwa majirani wetu,kwani suala zima la katiba ikiwemo mapendekezo ya kuwa na serikali tatu au serikali mbili yafanyike mezani na hili linawezekana",alisema Mhe Mbatia.

Aidha mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe akiwa ni mzungumzaji wa mwisho alisema,"Adui wa HAKI ni woga,sasa ili tushinde mapambano haya ya kudai haki ni lazima watanzania waondoshe woga,nachukuwa fursa hii kuliambia Jeshi la Polisi,tulikuwa tufanye maandamano ambayo ni haki yetu kikatiba,lakini mmetuzuwia,sasa mufahamu ya kwamba tarehe 10 october tutafanya maandamano makubwa na hatuwajibiki kuomba kibali bali tutawajibika kuwapa taarifa"mwisho wa kumnukuu.

AIdha alisema kama Rais atasaini muswada huo basi daima sisi wapinzania hatutoshiriki katika masuala yoyote ya kutunga sheria.

VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO IKIWA NI ISHARA YA MSHIKAMANO KATIKA KUDAI KATIBA NA TUME HURU.



Mwenyekiti wa Chama cha NCCR MAGEUZI MHE JAMES MBATIA alipokuwa anaongea jioni hii.




 MWENYEKITI WA CHADEMA AMBAYE PIA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI MHE FREEMAN MBOWE AKIHUTUBIA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI.


SEHEMU YA WANANCHI WALIOHUDHURIA KATIKA MKUTANO ULIOITISHWA NA VYAMA VYA UPINZANI.

0 comments:

Post a Comment