MKUTANO wa kujadili Rasimu ya Katiba Mpya ulioandaliwa na Chama
cha Wasioona wilayani Kahama umevunjika baada ya washiriki kususia
wakidai posho.
Mkutano huo ulivunjika siku ya pili baada ya wajumbe hao kutoka asasi
mbalimbali zisizokuwa za kiserikali wakiongozwa na baadhi kutoka kwa
Chama cha Walemavu wa Macho na Viungo, kukataa kuhudhuria mkutano huo
hadi Ofisa wa Ruzuku wa The Civil for Foundation Society, Ghati Horombe,
kutangaza kuwalipa posho hizo.
Tangazo la ofisa huyo liliongeza idadi ya washiriki kwa siku ya tatu
jambo lililomfanya Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye
Ulemavu wilayani Kahama, Maico Nkanjiwa aliwaonya kuacha tabia ya
kutanguliza maslahi katika masuala ya kujadili maisha yao.
Siku ya kwanza wajumbe zaidi ya 100 walihudhuria baada ya Nkanjiwa
kuwatangazia kuwa kusingelikuwa na posho isipokuwa wangelipata chai na
chakula cha mchana; jambo hilo lilizusha mzozo kwa washiriki hao wakidai
wasingeliwezi kushindia chakula.
Walisema wasingeliweza kula chakula huku familia zao zikiadhirika kwa
kushinda na njaa majumbani mwao na kudai kuwa ni vema wangeondoa gharama
za chakula, badala yake kuwalipa pesa, kuliko kuwashindisha hapo bila
malipo.
Kwa upande wake Horombe aliwataka Watanzania kuacha tabia hiyo kwa kuwa inaleta sura mbaya kwa wafadhili.
Hata hivyo mkutano huo ulimalizika kwa washiriki kuunga mkono uwepo wa
serikali tatu kwa madai kwamba serikali mbili haina maslahi kwa
Watanzania.
|
0 comments:
Post a Comment