Sep 11, 2013

Wazazi lawamani



 HUYU NI MMOJA KATI YA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.






Wazazi na walezi ni chanzo kikuu cha ongezeko la watoto waishio katika mazingira magumu hapa nchini.

Hayo yalisema na katibu wa kikundi cha Mtandao wa Marafiki wa Elimu Mwangaza, Ayub Bwanamad, alipozungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Pangani jana.

Alisema ugumu wa maisha kwenye baadhi ya familia unageuzwa sababu ya ongezeko la watoto hao huku akizitaka ofisi za kata kuweka utaratibu maalumu wa kuwasaidia.

Alishauri ofisi za wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutenga bajeti ya kuwasomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kupunguza changamoto huku akibainisha kwamba yapo maeneo mengine hayafikiwi.

Hata hivyo, Bwanamad ameitaka jamii kuacha kuwapa kazi ngumu na zenye kudhalilisha watoto kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi na kukiuka sheria.

Kwa mujibu wa katibu huyo kumjenga mtoto kwenye mazingira bora na kuwa karibu naye itapunguza wimbi hilo la watoto wanaoishi katika mazingira magumu huku akitoa wito kwa walezi na wazazi kuwapenda na kuwafundisha maadili mema watoto wao.
 
 HAWA NI SEHEMU YA WATOTO WANAOPATA MALEZI MEMA NA MATUNZO YA KARIBU KUTOKA KWA WAZAZI WAO.

0 comments:

Post a Comment