Sep 11, 2013

Rutto akana mashtaka



Naibu rais wa Kenya William Ruto amekana mashitaka ya uhalifu katika kesi inayoendeshwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC , Hague Uholanzi.

Bwana Ruto -- ambaye anatuhumiwa kupanga ghasia za baada ya uchaguzi uliokuwa na utata wa mwaka 2007 -- amekana mashtaka hayo sawa na mshitakiwa mwenza katika kesi hiyo mtangazaji Joshua Arap Sang.

Mwendesha mkuu wa mashtaka katika ICC, Fatou Bensouda, alimtaja Ruto kuwa mwanasiasa shupavu ambaye alipanga kufanya uhalifu dhidi ya binadamu ili kujinufaisha kisiasa.

Amesema kuwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Ruto aliunda jeshi lake la kivita kumpigania dhidi ya mahasimu wake madai ambayo yamekanushwa na wakili wa Ruto bwana Khan
Bwana Ruto na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang, wanatuhumiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, kufanya mauaji kuchochea na kupanga ghasia hizo.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, anatarajiwa kufikia katika mahakama hiyo mwezi Novemba

0 comments:

Post a Comment