MUFTI wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Issa Shaban bin
Simba amesema yeye si msanii kama anavyoshutumiwa na Mwenyekiti wa
Kamati ndogo ya Mazungumzo kati ya Waislamu na Serikali, Sheikh Suleiman
Kilemile.
Mufti Simba alisema
shutuma anazotupiwa zinatokana na malalamiko yake kwa Serikali kuhusu
kupuuzia suala la Mahakama ya Kadhi.
Kutokana na hali hiyo, Mufti Simba alisema yeye yupo sahihi na kwamba
anayemshutumu atumie sheria badala ya kulalamika kwenye vyombo vya
habari.
Simba alisema anachofahamu ni kwamba kupatikana kwa Kadhi hakuhitaji
ushirikishwaji wa taasisi zote za Kiislamu na kubainisha kuwa kama kuna
kosa lililofanyika sheria ndiyo itatengua kitendawili hicho na si
malalamiko.
“Huyo Sheikh Kilemile kama anadhani kulalamika ni dawa waulizwe
Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi na mimi sitaki kuendeleza mvutano
kwenye vyombo vya habari,” aling’aka Mufti Simba.
0 comments:
Post a Comment