WAFANYAKAZI wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) wamewasilisha
nyaraka kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harison Mwakyembe, ambazo
zilionyesha jinsi viongozi wao wanavyojinufaisha. Kitendo cha
kuwasilisha nyaraka hizo kilitokea Dar es Salaam jana na kilimfanya Dk.
Mwakyembe kutoa machozi na kushindwa kuongea.
Nyaraka hizo ziliwasilishwa na baadhi ya wafanyakazi zilionyesha
jinsi bidhaa zinavyosafirishwa kutoka Tanzania kwenda Jamhuri ya
Demokrasia ya Congo (DRC) huku kiasi kikubwa cha mapato kikibakia
mifukoni mwa vigogo wa TAZARA.
Katika mkutano huo, wafanyakazi hao waliwasilisha taarifa za Mkurugenzi mpya wa Shirika hilo kuishi katika Hoteli ya New Afrika wakati nyumba anayotakiwa kuishi ikiwa imepangishwa na mkurugenzi aliyemaliza muda wake.
Wafanyakazi hao waliwasilisha nyaraka zinazotumika kusafirisha bidhaa kwa kupunguza bei badala ya gharama halisi inayotakiwa na fedha nyingine wanazichukua viongozi wao.
Aidha, wafanyakazi hao walimueleza Dk. Mwakyembe kuwa TAZARA ina madeni makubwa ambayo hayajawahi kuzungumzwa na kuwekwa wazi yaweze kulipwa na badala yake wamekuwa wakisingizia kwamba wafanyakazi wanadai.
Walimueleza kuwa mameneja saba waliofukuzwa wamerejea kazini na hatua hazijachukuliwa kama zilivyoelekezwa na Baraza la Mawaziri kuwa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua za kisheria na badala yake wameendelea kufanya kazi kwa kuharibu vielelezo na nyaraka nyeti.
Mfanyakazi Amiri Husein alisema kuna mabehewa 26 yalipelekwa DRC lakini fedha zake ziliishia mifukoni mwa wakubwa.
Alisema Julai 25, 2013, treni ilipakia mafuta kutoka Tanzania kwenda DRC ambapo zaidi ya Sh bilioni moja iliyolipwa iliishia mifukoni mwa wajanja.
Akijibu malalamiko ya wafanyakazi hao, Dk. Mwakyembe, aliiagiza menejimenti ya TAZARA kutoa maelezo kutokana na tuhuma zilizotolewa.
Aliwataka wafanyakazi kurejea kazini leo na wafanye kazi kwa ueledi na ufanisi mkubwa kwa ajili ya kufidia hasara ya Sh bilioni 2.4 iliyotokea wakati wa mgomo.
Alisema TAZARA inafanya kazi kwa hasara na inafilisika na kwamba Tanzania na Zambia zimekaa pamoja kuinusuru.
Alisema mapato ya TAZARA kwa mwezi ni Sh bilioni 2.4 wakati matumizi ni Sh bilioni nne na mambo hayo yanatokana na ufanisi mbovu wa kiutendaji na kutochukua uamuzi mzito.
“Kutokana na yote hayo, Tazara itachukua muda mrefu kurejea katika hali yake ya kawaida,” alisema Dk. Mwakyembe.