Sep 25, 2013

Polisi Burundi yazingira mitaa ya Waislamu


Kwa mujibu wa Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW mjini Bujumbura, Amida Issa, anaripoti kuwa polisi ya taifa ya Burundi iliuzingira mtaa wa Buyenzi mjini Bujumbura na Rumonge mkoani Bururi alfajiri ya Jumatano.

Kuuzingira mtaa huo kunatokana na kile ilichosema ni kuwasaka wapiganaji wa Al-Shabaab na wanaowaunga mkono. 

Mitaa hiyo yote ina wakaazi wengi ambao ni Waislamu. 

Burundi ni miongoni mwa mataifa yaliyo na wanajeshi wake nchini Somalia.

0 comments:

Post a Comment