
Kenya
inaanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa waathiriwa wa
mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la
Westgate mjini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta pia ameseama kuwa bendera
zitapepershwa nusu mlingoti kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika
mashambulizi hayo.
Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na
wale wa Kenya kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya
jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana.
Nia ni kujaribu pia
kutambua uraia wa washambulizi hao.
Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.
Magaidi watato wa kundi la Al Shabaa lililokiri
kutekeleza mashambulizi hayo,waliuawa katika shambulizi hilo lililodumu
siku nne na kuwa washukiwa wengine 11 walikamatwa wakijaribu kuondoka
nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano ,
Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na kuwa Kenya
imejeruhiwa vibaya,lakini alielezea matumaini kwa kuwa shambulizi
limeisha na kusema kwamba waliohusika watakiona cha mtemakuni.
Wakati huohuo, afisaa mmoja mkuu wa serikali ya
Somalia, amesema kuwa hakuna suluhu la kijeshi kwa kundi la wanamgambo
wa Al Shabaab nchini humo. Wanamgambo hao wameitikia kuhusika na
mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya ambao watu zaidi ya sitini
wameuawa.
0 comments:
Post a Comment