Mtoto Emily akiwa Hospitalini kwa matibabu
WIMBI
la ukatili dhidi ya watoto linazidi kushika kasi jijini mkoani mbeya baada ya
mtoto, Emilly George (7) Mkazi wa kijiji cha Ruanda wilaya ya Mbeya
kuunguzwa vibaya mikono na mama yake mzazi, Elisia Mwasile (41) kwa maji
ya moto kisha kufungiwa ndani kwa siku saba.
Akizungumza huku akiwa anatetemeka kwa hofu, mama wa mtoto huyo, Elisia alisema kuwa chanzo cha kumchoma mtoto wake ni kutokana na kuchoshwa na malalamiko ya majirani zake waliokuwa wakimtuhumu mtoto huyo kujihusisha na vitendo vya wizi vya kuiba fedha na mayai ya kuku.

Tukio
la mwisho lililosababisha mtoto huyo kuchomwa na maji ya moto ni la
hivi karibuni ambapo majirani walimwambia mama huyo kwamba mtoto wake
ameiba mayai kutoka kwa majirani zake.
Baada ya kuunguzwa kikatili, mtoto huyo alifungiwa ndani kwa siku saba bila matibabu yoyote hali iliyowafanya majirani kuanza kumtafuta wasijue alipo.
Baada ya kutomuona mitaani, majirani hao walitoa taarifa ofisi ya kijiji ili kubaini alipo mtoto huyo.
Uongozi wa kijiji baada ya kupata taarifa hizo ulifanya upekuzi na kumkuta mtoto huyo akiwa amefungiwa ndani huku akiwa na majeraha makubwa katika mikono yake ndipo taarifa ilitolewa Kituo cha Polisi Mbalizi na mama huyo kukamatwa.
Baada ya kukamatwa mama huyo alikabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia na Watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya, Pudensiana Baitu na mwenyekiti wake, Mary Gumbo ambaye muda mwingi alikuwa akiangua kilio kutokana na kitendo alichofanyiwa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo ni kwamba mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa akihojiwa na
Polisi Kituo Kikuu cha jijini Mbeya na anatarajiwa kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Mtoto Emilly amelazwa katika Hospitali ya Rufaa wodi namba tano akiendelea kupatiwa matibabu.
Vitendo vya unyanyasaji vimeendelea kukemewa jijini Mbeya na asasi mbalimbali kutokana na watoto kubakwa, kulawitiwa, kufanyishwa kazi za ndani na baadhi yao kupata ulemavu wa kudumu ikiwemo kupoteza viungo.
0 comments:
Post a Comment