Aug 4, 2013

TAASISI YA MUNIIRA MADRASA YAISHUKURU AMANA BENK.


 Na mwandishi wetu wa munira.
Taasisi ya muniira madrasa yenye makazi yake magomeni makuti jijini Dar es salaam imeishukuru benk ya Amana kwa kuisaidia taasisi hiyo kufanikisha futari ya pamoja kwa lengo la kuwafariji wajane,yatima,wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Shukrani hizo zilitolewa jana na Ustaadh Juma Rashid ambaye ni katibu mkuu wa taasisi hiyo alipokuwa anatoa tamko la shukrani muda mfupi kabla ya dua.

"Tunawashukuru wazazi kwa michango yenu mbalimbali,tunawashukuru watu binafsi ambapo si rahisi kuwataja wote,lakini pia shukrani maalumu ziwaendee ndugu zetu wa Amana Benk ambao wametusaidia kwa kiasi kikubwa sana kufanikisha tukio hilo,ALLAH awabariki na awape kila la kheri katika kazi zao,alisema.


Pia aliwashukuru wote waliohudhuria huku akiwaomba radhi pale penye mapungufu.

Aidha kupitia futari hiyo katibu mkuu Ustaadh Juma Rashid aliwaomba wazee,wajane,yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kufika ofisini hapo siku ya tarehe nne mwezi huu ili kukabidhiwa misaada yao iliyotafutwa na taasisi hii.

Pia alitumia nafasi hiyo kutangaza kwamba kwa akina mama wanaotaka kujiunga na masomo ya ushonaji, kudarizi na mapambo wafike kwa ajili ya kujiandikisha,aidha wanaohitaji kujiunga uanachama katika taasisi hiyo wachukuwe fomu ambapo watu kadhaa walijitokeza papo hapo kuchukua fomu hizo.
KATIBU MKUU USTAADH JUMA RASHID AKITOA TAMKO LA SHUKRAN MARA  BAADA YA KUFUTURISHA



 SEHEMU YA WAUMINI WAKIFUTURU KATIKA FUTARI YA PAMOJA ILIYOANDALIWA NA TAASISI YA MUNIRA MADRASA HAPO JANA.